Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah
Mchechu (Kushoto aliyekaa) akisaini hati za makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya NBC,Lawrence Mafuru  kuhusu suala la mikopo ya nyumba jijini Da es
Salaam leo, Wanaoshuhudia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Injinia
Kesogukewele Msita.
Tunapenda kumpongeza kwa dhati kabisa kiongozi huyu kijana ambaye ameweza kuliweka shirika hili la Nyumba la Tanzania ambalo kwa mtazamo wa haraka haraka lilikuwa kama linakwenda kufa kama yalivyokufa mashirika mengine hapa nchini, KAPINGAZ Blog kwa kutambua mchango wako mkubwa ambao unautoa katika jamii yetu ya watanzania ambao wengi wetu tunaishi katika maisha duni ambayo hayaonekani mbele wala nyuma, jamii kubwa ya Watanzania wanaishi nyumba za kupanga ambazo hazina uhakika katika maisha ya mpangaji. 
Kwa kutambua na kuheshimu mawazo yako ambayo uliwahi kuyatoa katika mikutano yako ya kusema nitakunukuhu, ” hakuna Shirika duniani ambalo ni tajiri kama shirika linalomiliki nyumba” ni cha hajabu sana kuona shirika letu limekuwa likiyumba ili hali lina rasilimali nyingi ambazo wangeweza kuzitumia vizuri zingeweza kuwasaidia wote kwa ujumla wao na wanachi wakafaidi matunda ya rasilimali zao. 
Tunakuomba usikatishwe wala kuvunjwa moyo na watanzania wachache wasioitakia mema Nchi yetu na hasa watanzania walio wanyonge ambao hawajui mkombozi wao atakuja lini, sisi tupo nyuma yako.
source:http://kapingaz.blogspot.com/